Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Clement Sangu, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kazi wa Qatar, Mhe. Dkt. Ali bin Saeed bin Samikh Al Marri, Jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Katika mazungumzo ya viongozi hao, pande zote zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kazi na ajira, ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu, kukuza fursa za ajira na kulinda haki za wafanyakazi.
Vilevile, Ushirikiano huo umelenga kupanua fursa za ajira kwa Watanzania na kuendelea kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Qatar.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Clement Sangu, akizungumza na Waziri wa Kazi wa Qatar, Mhe. Dkt. Ali bin Saeed bin Samikh Al Marri, walipokutana katika kikao cha pembeni (side meeting) wakati wa mkutano wa Mawaziri wa Kazi (Global Labour Market Cinference) unaofanyika Jijini Riyadh, Saudi Arabia.


0 Comments