Ticker

6/recent/ticker-posts

OSHA YAJA NA MPANGO WA KUWEZESHA BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akizungumza na washiriki wa kikao kazibaina ya OSHA na Maafisa Biashara wa Mikoa na Wilaya za Kanda ya Kaskazini(hawapo pichani).

***************

Na Mwandishi Wetu

Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umezindua mpango wake wakushirikiana na Maafisa Biashara wa Mikoa na Wilaya katika kuwezesha biashara nauwekezaji nchini.

Mpango huo unahusisha utaratibu wa kuunganisha mifumo na kubadilishana taarifa za biashara na miradi mbalimbali ya uwekezaji ili kurahisisha ufikishaji wa huduma za urasimishaji biashara na ukaguzi wa mifumo ya usalama na afya mahali pa kazi.

Mpango huo wa OSHA umewekwa wazi na Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Khadija Mwenda, alipohitimisha semina ya kujenga uelewa wa pamoja baina ya OSHA naMaafisa Biashara wa Mikoa na Wilaya zote za Kanda ya Kaskazini ambao umefanyikakwa siku moja katika Ofisi za OSHA zilizopo Jengo la PAPU Jijini Arusha.

Bi.Mwenda amesema mpango huo umeibuliwa ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa akielekeza Taasisi za serikalikushirikiana katika utendaji ikiwemo kuhakikisha kwamba mifumo mbalimbali ya serikaliinasomana.

Aidha, ameeleza kuwa mpango huo unalenga kutekeleza agizo la Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Deus Sangu, alilolitoa Desemba 22, 2025 ambapo aliwataka waajiri/wamiliki wa maeneo ya kazi kote nchini kuhakikisha maeneoyao ya kazi yanasajiliwa OSHA ndani ya siku 90 kuanzia mwezi Januari 2026 ilikurahisisha usimamizi wa masuala ya usalama na afya katika maeneo husika.

“Lengo kuu la mpango huu ni kuhakikisha kuwa Taasisi ya OSHA inafanya kazi kwakushirikiana na wenzetu ambao ni Maafisa Biashara wa Mikoa na Wilaya wote tukiwakama Taasisi wezeshi katika biashara na uwekezaji,” ameeleza Mtendaji Mkuu waOSHA na kuongeza:

“Tumekuwa na kikao kizuri sana ambacho kimetufungulia zoezi letu ambalo tumepangakulifanya nchi nzima. Mpango huu utakapokamilika sote tutakuwa na uelewa wa pamojaambao utapelekea taasisi zetu kuwa wawezeshaji zaidi badala ya kuwa wadhibiti washughuli za biashara na uwekezaji nchini.”

Kwa upande wao washiriki wa semina hiyo ambao ni Maafisa Biashara wa Mikoa naWilaya zote za Kanda ya Kaskazini ikihusisha mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga, wamepongeza mpango huo na kuahidi kushirikiana na OSHA kufanikishampango huo.

“Tumefurahia sana mafunzo ya leo,hakika tumetoka na ufahamu mpana kuhusiana nakazi za OSHA na tumeona kuna umuhimu mkubwa sana kwa wafanyabiashara nawawekezaji kujisajili katika mfumo rasmi ili waweze kuweka salama sehemu zao za kazi,” ameeleza Bw. Elisha Erasto, Mkuu wa Idara ya Biashara wa Halmashauri yaWilaya ya Rombo.

“Tunaishukuru sana OSHA kwa semina ya leo na kwaniaba ya washiriki wenzanguninapenda kusema kwamba tutashirikiana na OSHA ili kufanikisha mpango huuunaolenga kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini na hivyo kufanikishamalengo ya Dira ya Taifa 2050,” amesema Bi. Lulu Kaaya, Afisa Biashara Mkoa waArusha.

OSHA ni Taasisi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) yenye jukumula kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003inayoweka utaratibu wa kitaifa wa usimamizi wa masuala ya usalama na afya katikamaeneo ya kazi.

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akizungumza na washiriki wa kikao kazibaina ya OSHA na Maafisa Biashara wa Mikoa na Wilaya za Kanda ya Kaskazini(hawapo pichani).
Meneja wa Usalama Mahali pa Kazi wa OSHA, Mhandisi Robert Mashinji, akiwasilishamada kuhusu usajili wa maeneo ya kazi na utekelezaji wa majukumu ya OSHA kwaujumla katika kikao kazi baina ya OSHA na Maafisa Biashara wa Mikoa na Wilaya za Kanda ya Kaskazini.
Meneja wa Kitengo cha Sheria OSHA, Bi. Pendo Berege, akiwasilisha mada kuhusuSheria Na. 5 ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 katika kikao kazibaina ya OSHA na Maafisa Biashara wa Mikoa na Wilaya za Kanda ya Kaskazini.

Washiriki wa kikao kazi baina ya OSHA na Maafisa Biashara wa Mikoa na Wilaya za Kanda ya Kaskazini wakifuatilia mawasilisho toka kwa wataalam wa OSHA kuhusuSheria na Usalama na Afya Mahali pa Kazi pamoja na utekelezaji wa majukumu yaOSHA kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments