Ticker

6/recent/ticker-posts

TANGA KUNUFAIKA NA MRADI WA "SCHOOL WaSH" CHINI YA UFADHILI WA ROTARY KUTOKA UHOLANZI.





Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga(TangaUWASA) imeingia makubaliano maalum na taasisi ya ROTARY inayofanya kazi kwa kushirikiana na Mamlaka za Maji Nchini Uholanzi (VEi) ya kutekeleza mradi wa kuwezesha huduma za kijamii mashuleni kupitia ujenzi wa vyoo (SCHOOL WaSH) kwa shule za msingi katika Jiji la Tanga.


Akizungumza kwa niaba ya uwakilishi wa ROTARY Bi.Emma Lesterhuis ameainisha kuwa mradi huo utatekelezwa na TangaUWASA kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Tanga na utajikita zaidi katika ujenzi wa vyoo kwa baadhi ya shule zenye idadi kubwa ya wanafunzi na uhaba wa matundu ya vyoo.


Nae kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TangaUWASA, Mha. Geofrey Hilly amewashukuru ROTARY kwa kutambulisha mradi huo ambao unaenda kuwezesha jamii hususani wanafunzi kupata huduma muhimu na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha wakati wote wa utekelezaji wa mradi na usimamizi wake.










Tanga unakuwa Mkoa wa tatu nchini kunufaika na mradi wa "SCHOOL WaSH" ukiungana na Mikoa ya Arusha na Mwanza ambayo utekelezaji wake unaendelea.

Post a Comment

0 Comments