Ticker

6/recent/ticker-posts

Kwa Nini Bolt Inaendelea Kuongoza Soko la Usafiri wa Kidijitali Tanzania


Ivi karibuni, ujumbe wa uongozi wa Bolt Tanzania uliwasilishwa kwa namna ya kipekee si jukwaani, bali ndani ya duka dogo la mfanyabiashara mwanamke wa Kitanzania.

Katika mahojiano ya ana kwa ana na mtangazaji wa zamani wa BBC, Salim Kikeke, Meneja Mkuu Mwandamizi wa Bolt Afrika Mashariki, Dimmy Kanyankole, alieleza sababu zinazoifanya Bolt kuendelea kufanya vizuri nchini, akibainisha kuwa uongozi wa soko haujengwi tu kwa mapato, bali kwa athari chanya kwa jamii.

Mahojiano hayo yalifanyika katika duka la mfanyabiashara kijana mwanamke eneo la Mikocheni, jambo lililoimarisha hoja ya Bolt kwamba usafiri ni miundombinu ya uchumi.

Wakati watu na bidhaa wanaposafiri kwa uhakika, biashara ndogo na za kati hupata wateja, wafanyakazi hupata fursa, na miji huendesha shughuli zake kwa ufanisi zaidi.

Kanyankole alisisitiza kuwa mafanikio ya Bolt yanabebwa na jumuiya ya madereva wake zaidi ya madereva washirika 30,000 nchini wanaotegemea jukwaa hilo kwa kipato cha kila siku. Katika muktadha huo, uendelevu si kauli ya kibiashara bali ni suala la ustawi wa maisha

“Bolt inafanya kazi katika zaidi ya nchi 50 duniani, na mwaka 2025 Tanzania ilikuwa miongoni mwa masoko yanayokua kwa kasi zaidi barani Afrika, na ya pili duniani baada ya Uswisi,” alisema, akihusisha ukuaji huo na ongezeko la mahitaji ya suluhu jumuishi za usafiri wa kidijitali.

Mtazamo huo wa athari kwa jamii ulijitokeza pia katika hafla ya Africa Transportation Excellence Awards 2026 iliyofanyika mapema mwezi Mei jijini Dar es Salaam, ambapo Bolt Tanzania ilitunukiwa tuzo ya Kampuni Bora ya Usafiri wa Mijini na Ride-Hailing kwa Mwaka.

Katika hotuba yake, Kanyankole aliipongeza serikali na wadhibiti kwa kuweka mazingira thabiti ya ukuaji, akieleza kuwa ubunifu endelevu hustawi pale sera na sekta binafsi zinaposhirikiana.

Alitoa tuzo hiyo wakfu kwa madereva injini halisi ya uchumi wa usafiri wa kidijitali unaokua kwa kasi nchini Tanzania.

Aidha, kampuni hivi karibuni iliongeza nauli kwa kuzingatia tangazo rasmi la LATRA, hatua iliolenga kulinda mapato ya madereva dhidi ya athari za ongezeko la bei za mafuta ambalo limeongezeka maradufu tangu Machi 2026.

Post a Comment

0 Comments