Ni kauli yake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), anayeshugulikia Afya, Dkt. Rajabu Seif, alipotembelea banda la NEMC viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre, Jijini Dodoma kwenye maonesho ya kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika 05/06 Kila Mwaka ambayo kwa mwaka huu yanakaulimbiu isemayo Dira 2050: Tuwajibike Kukijanisha Tanzania.
Akiwa katika banda hilo, Dkt. Seif alipongeza juhudi za NEMC katika kuelimisha wananchi kuhusu masuala ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira nchini.
Alisema kazi inayofanywa na NEMC ina mchango mkubwa katika kuongeza uelewa wa jamii kuhusu wajibu wao wa kulinda mazingira na kuhakikisha rasilimali za asili zinatunzwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Katika banda hilo, wananchi wanapata elimu kuhusu umuhimu wa kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii, umuhimu wa upandaji miti, utenganishaji wa taka kuanzia kwenye chanzo, pamoja na dhana ya taka sifuri inayolenga kupunguza uzalishaji wa taka na kuongeza matumizi ya mbinu za urejelezaji.
Dkt. Seif alisisitiza kuwa ushirikiano kati ya NEMC, taasisi mbalimbali na wananchi ni muhimu katika kufanikisha agenda ya uhifadhi na usimamizi endelevu wa mazingira nchini inafanikiwa kwa maendeleo endelevu




0 Comments