Ticker

6/recent/ticker-posts

OFISI YA WAZIRI MKUU NA TAASISI YA CHAKULA NA LISHE TANZANIA KUSHIRIKIANA KUANDAA MPANGO WA LISHE TAIFA






Na Mwandishi Wetu- Dodoma

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Bi. Debora Charwe amesema, Serikali ipo katika mchakato wa kuandaa Mpango wa Muda Mrefu wa Lishe wa Taifa (NN-LTP) ili kuongeza jitihada za sekta mtambuka katika kuboresha utekelezaji wa lishe kwa kipindi cha miaka 25 ijayo

Bi. Debora ameyasema hayo leo tarehe 30 Juni, 2026 wakati akifungua Warsha ya mafunzo kuhusu kuandaa mpango wa muda mrefu wa lishe wa Taifa (National Nutrition Long Term Plan 2026-2050) ambayo inafanyika jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Juni 30 hadi Julai 02, 2026



Amesema, mafunzo hayo yanatolewa kwa Wataalam kutoka ngazi ya Wizara mbalimbali kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu uandaaji wa mipango ya muda mrefu wa lishe inayojumuisha sekta mtambuka pamoja na kubadilishana uzoefu kusaidia katika usanifu, muundo na taratibu za utekelezaji wa Mpango wa muda mrefu wa Lishe wa Taifa.




















Vilevile Bi. Debora amefafanua kuwa, mpango huo unaandaliwa chini ya usimamaizi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) na wadau wengine wa maendeleo kwa kuzingatia haja ya kuifanya lishe kuwa moja ya kichocheo na kipimo katika kufikiwa kwa malengo ya Dira ya Maendeleo ya Tanzania kufikia 2050.

Aidha, warsha hiyo imehusisha Afisa viungo wa lishe kutoka Wizara mbalimbali zikiwemo Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) pamoja na Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Viwanda, Wizara ya Maji na Wizara ya Mambo na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Post a Comment

0 Comments