KAHAMA
Baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) limetoa wito kwa wananchi wa manispaa ya Kahama hususan wakazi wa kata ya Mwendakulima kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo katika kituo cha mafunzo ya kilimo kilichopo kata ya mwendakulima wilayani Kahama mkoani Shinyanga kilicholenga kuwainua wananchi katika sekta ya kilimo.
Akizungumza baada ya kutembelea kituo hicho Mkurugenzi wa uwezeshaji na Ushiriki wa watanzania Neema Mwakatobe amesema kuwa wametembelea kituo hicho na kuona fursa nyingi zinazopatikana katika kituo hicho.
“Tunashukuru kwa mwaliko huu ambao umetufanya tufike hapa,tumetembelea kituo hiki na tumeona fursa mbalimbali zinazopatikana katika kituo hiki ambazo zinaweza kuwainua wananchi kiuchumi,tumeona maeneo yenye changamoto na tumeweka mikakati na manispaa ya Kahama ya kuweza kuimarisha kituo hiki,hivyo wananchi wanatakiwa kuchangamkia fursa kituo hiki” Amesema Mwakatobe.
Katika hatua nyingine Bi Mwakatobe amesema kuwa baraza la taifa la uweshaji wananchi Kiuchumi lina jukumu la kuhakikisha kituo cha Mwendakulima kinaenda mbele na kuwasaidia wananchi katika mipango ambayo imepangwa katika kituo hicho.
“Yote ambayo mmezungumza kama changamoto majiu yake yapo ndani ya serikali nan je ya serikali na sisi kama baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi tuna jukumu kubwa la kuhakikisha kituo hiki kinaendelea na kinawanufaisha wananchi wa Mwendakulima na Manispaa ya Kahama kwa ujumla” Ameongeza Bi Mwakatobe.
Awali akitoa taarifa ya kituo hicho mkuu wa divisheni ya Kilimo,mifugo na uvuvi manispaa ya Kahama Richard Yegele amesema kuwa lengo la kituo hicho ilikuwa kuwapa mafunzo wananchi kama shamba darasa ili waende kulima mashama makubwa kupitia mafunzo waliyopata katika kituo hicho.
“Huu mradi ulianza miaka kumi iliyopita lengo lilikuwa ni kutoa elimu kama shamba darasa kwa wakulima na kisha wakulima Kwenda kulima mashamba makubwa baada ya kupata elimu hii,lakini kadri siku zinavyoenda tukaona tuongeza shughuli nyingine za kiuchumi a sasa tuna mashine ya kukuboa mpunga Pamoja na mashie ya kukamua mafuta ya alizeti,na sasa kituo kinaendeshwa na ushirika (AMCOS)” Amesema Yegele.
Akielezea changamoto zinazokikabili kituo hicho Meneja wa chama cha ushirika Mwendakulima Prisca Aron amesema kuwa kituo kinakabiliwa na upungufu wa mtaji wa kununua mazao,Uchakavu wa mitambo Pamoja na kuezuliwa kwa paa la kitalu nyumba.
“Katika kituo chetu tunakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa fedha za mtaji kwa ajili ya kununua mazao,Uchakavu wa mitambo ya kukoboa Mpunga na kuezuliwa kwa paa la kitalu nyumba hali iliyosaabisha kilimo chaa kitalu nyuma kusimama” Amesema Bi Aron.









0 Comments