Ticker

6/recent/ticker-posts

MHAGAMA AKEMEA MILA NA DESTURI POTOFU KWA WANAWAKE NA WATOTO


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wakati wa ufunguzi wa kikao cha Kamati Elekezi ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto katika Ukumbi wa Hoteli ya Nashera Mkoani Morogoro tarehe 22 Oktoba, 2021.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda akieleza kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) wakati wa kikao cha Kamati Elekezi ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto katika Ukumbi wa Hoteli ya Nashera Mkoani Morogoro.


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akichangia jambo wakati wa kikao cha Kamati Elekezi ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto, katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro na kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio.


Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Kamati Elekezi ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto wakifuatilia kikao hicho.


Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Kamati Elekezi ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto wakifuatilia kikao hicho.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Tixon Nzunda (Kulia) pamoja na Katibu ya Kamati Elekezi ya Masuala ya MTAKUWWA Bw. Sayi Magessa (kushoto) wakifuatilia kikao hicho.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju akifafanua masuala ya kisheria wakati wa kikao hicho.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Makatibu Wakuu wakiwa katika picha ya pamoja na sekretarieti ya Kamati ya Elekezi ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto.Kulia kwa waziri ni Katibu Mkuu wa ofisi yake, Bw. Tixon Nzunda, kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, wa tatu kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio na wa tatu kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

********************************

MWANDISHI WETU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameitaka jamii kubadili mitazamo kwa kuhakikisha inapinga mila na desturi zilizopitwa na wakati zinazokandamiza wanawake na watoto nchini.

Ameyasema hayo alipofungua kikao cha Kamati Elekezi ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa,Wakuu wa Taasisi pamoja na Asasi za Kiraia katika Ukumbi wa Hoteli ya Nashera Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.



Waziri alisema ni wakati sahihi kwa jamii kubadili mitazamo na kupinga mila na desturi zinazowagandamiza wanawake na watoto na kupelekea kuathiri katika maeneo mbalimbali..

“kumekuwepo na mila na desturi potofu ndani ya jamii zetu zikiwemo za ukeketaji na ndoa za utotoni ambazo zimeendelea kumkosesha haki na kuathiri maendeleo na ustawi wa mtoto wa kike”alisisitiza.



Waziri Mhagama alisema Serikali imeendelea kuweka mikakakti kuhakikisha inatokomeza masuala ya ukatili dhidi ya Wananwake na Watoto nchini kwa kupinga vitendo vya kikatili kwa makundi hayo pamoja na kuweka sheria na kanuni zitakazoainisha namna bora ya kupambana na vitendo hivyo.

Aidha, mila na desturi potofu zimechangia vitendo vya ukatili dhidi makundi hayo ambapo vimechangia kukwamisha jitihada za kuelekea usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake hivyo zinahitajika jitihada endelevu za pamoja baina ya serikali na wadau.



Alisema yapo madhara mengi yatokanayo na vitendo vya ukatili kwa makundi hayo ikiwemo kuwakosesha haki ya ushiriki katika shughuli za uzalishaji na kujiletea maendeleo yao na jamii kwa ujumla.

.

“Wote tunatambua madhara ya vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa Taifa yakiwemo ya kiuchumi, kiafya na kijami,ukatili kwa watoto hususan unaofanywa na watu au ndugu wa karibu umekuwa na athari mbaya zaidi kwa ustawi na maendeleo ya watoto nchini,”alieleza waziri Mhagama.

Aliongezea kuwa, katika kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto hapa nchini serikali kwa kushirikiana na wadau imewezesha uwanzishwaji wa madawati ya jinsia na watoto katika vituo vya polisi.



“Hadi kufikia mwaka 2020/2021 jumla ya madawati 420 yameanzishwa katika vituo mbalimbali vya polisi hapa nchini aidha jitihada za kukabiliana na vitendo vya ukatili katika vyuo vya elimu ya juu na kati zimeendelea ambapo hadi kufikia februari, 2021 jumla ya madawati matano ya jinsia yameanzishwa katika taasisi za elimu ya juu na kati”, alisema.



Sambamba na hilo alieleza katika kuimarisha ulinzi na usalama wa wanawake na watoto nchini, jumla ya Kamati 18,186 za Ulinzi wa Wanawake na Watoto zimeanzishwa katika ngazi ya Mkoa, Halmashauri, Kata na Kijiji/Mtaa mwaka 2020/21 ikilinganishwa na Kamati 16,343 mwaka 2019/20, sawa na ongezeko la Kamati 1,843.



“Nafahamu Mpango wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) unalengo la kupunguza ukatili kwa wanawake na watoto kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2021/22 ili kufikia lengo hilo serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imekuwa ikitekeleza afua mbalimbali zinazolenga kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kupitia maeneo nane ya utekelezaji”,amesema.



Waziri aliendelea kuhimiza Kamati hiyo Kuhakikisha rasilimali fedha kwa ajili ya utekelezaji wa afua za MTAKUWWA zinatengwa na kutolewa kwenye Wizara na Taasisi husika, kuandaa mikakati madhubuti itakayosaidia kuimarisha utendaji wa Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto kwenye ngazi zote na Kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa taarifa za ukatili nchini kwa lengo la kubaini ukubwa wa tatizo na kulitafutia ufumbuzi stahiki.



Waziri aliongezea kuwa ni vyema Kuendelea kubaini kada zenye upungufu mkubwa wa watendaji hususan katika ngazi ya kata na vijiji ili kuwezesha ufanisi katika utekelezaji wa mpango huo pamoja na kushughulikia changamoto za sheria na kijamii zinazotoa mianya ya watuhumiwa wengi wa kesi za ukatili kuachiwa huru.

Post a Comment

0 Comments