***************************
Na Magrethy Katengu
Serikali kupitia Shirika la Maendeleo Nchini (NDC) imesema itahakikisha inaboresha mazingira ya uwekezaji wa Viwanda ili kuwafanya wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wavutiwe kuwekeza miradi mbalimbali itakayo chochea ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa Ujumla.
Hayo yamesemwa Leo na Mkurugenzi mtendaji wa Shirika Hilo Nicholaus Shombe wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelezea mikakati iliyojiwekea katika kuhakikisha NDC inawanufaisha wawekezaji katika masuala ya Uwekezaji wa Viwanda.
Aidha amesema Kwamba NDC kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini( TANESCO) wameanza kutatua kero ya kukatika kwa umeme Mara kwa Mara,pamoja nakuimarisha mfumo wa upatikanaji wa maji ya uhakika ili kuwafanya wawekezaji wawe na mazingira bora ya Uwekezaji.
Dr.Shombe amewaomba Watanzania waendelee kuliamini Shirika lao la Maendeleo la Taifa(NDC) kwasababu lina miradi mikubwa ambayo inatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa ya viwanda nakwamba tayari kuna baadhi ya wawekezaji kutoka mataifa yakigeni yameonyesha nia yakuwekeza katika viwanda vya kuunganisha magari.
"Tuna miradi mingi mikubwa ambayo tunaitekeleza,kuna Mradi wa Magadi Soda Mradi huu nimkubwa sana,ukizungumzia Makemoko ya Viwanda unazungumzia Magadi soda ,hivyo nawaomba Watanzania waendelee kuliamini Shirika lao la Maendeleo, namimi nikiwa kama mkurugenzi mtendaji kwa kushirikiana na timu yangu tutahakikisha tunaleta mabadiliko makumbwa ndani ya shirika " amesema Dr.Shombe.
Nakuongeza kwamba "Tunataka tuwe na NDC yatofauti, shirika lipo kwa ajili yakuwasaidia watanzania,na maadhimisho haya ya siku ya mwanamke Duniani tupo hapa kuwambia wanawake kwamba NDC ipo kwa ajili yao ,wachangamkie firsa ya uwekezaji wa viwanda.
Dr. Shombe amewataka wanawake kuelekea maadhimisho yasiku ya mwanamke Dunia inayoazimishwa Machi 8 kila mwaka ,wajitokeze kuchangamkia fursa ya uwekezaji wa viwanda vya nguo kwenye kongani ya Viwanda ya NDC iliyopo kibaha Mkoani Pwani ili kuwafanya wanawake wazawa wanufaike na Viwanda.
Dr.Shombe ambaye ametembelea maonyesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wanawake kupitia viwanda vidogo ambayo yanafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam,ambapo amefurahishwa na kazi kubwa wanayoifanya.
0 Comments