Ticker

6/recent/ticker-posts

HESLB KUWADAI SHILINGI 10.6 BILIONI WALIOKOPESHWA LAW SCHOOL OF TANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Bw.Abdul-Razaq Badru akiwa pamoja na Mkuu wa Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Jaji Dkt. Benhajj Masoud wakisaini mkataba wa makubaliano HESLB kudai waliokopeshwa Law School of Tanzania. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 21,2022 katika Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Bw.Abdul-Razaq Badru akipeana mkono wa pongezi na Mkuu wa Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Jaji Dkt. Benhajj Masoud mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano HESLB kudai waliokopeshwa Law School of Tanzania. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 21,2022 katika Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Bw.Abdul-Razaq Badru akiwa pamoja na Mkuu wa Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Jaji Dkt. Benhajj Masoud mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano HESLB kudai waliokopeshwa Law School of Tanzania. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 21,2022 katika Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Bw.Abdul-Razaq Badru akizungumza wakati wakisaini mkataba wa makubaliano HESLB kudai waliokopeshwa Law School of Tanzania. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 21,2022 katika Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Jaji Dkt. Benhajj Masoud akizungumza wakati wakisaini mkataba wa makubaliano HESLB kudai waliokopeshwa Law School of Tanzania. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 21,2022 katika Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Bw.Abdul-Razaq Badru akizungumza jambo na Mkuu wa Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Jaji Dkt. Benhajj Masoud wakati wakisaini mkataba wa makubaliano HESLB kudai waliokopeshwa Law School of Tanzania.Hafla hiyo imefanyika leo Juni 21,2022 katika Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Jijini Dar es Salaam Baadhi ya watumishi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wakiwa kwenye hafla ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano kati ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) kuwa HESLB kudai waliokopeshwa Law School of Tanzania. Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) wakiwa kwenye hafla ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano kati ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) kuwa HESLB kudai waliokopeshwa Law School of Tanzania.Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Bw.Abdul-Razaq Badru akiwa pamoja na Mkuu wa Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Jaji Dkt. Benhajj Masoud wakipata picha ya pamoja na watumishi wa HESLB pamoja na LST wakati wakisaini mkataba wa makubaliano HESLB kudai waliokopeshwa Law School of Tanzania. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 21,2022 katika Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*****************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WANASHERIA 5,025 waliokopeshwa zaidi ya Shilingi Bilioni 10.6 kama mikopo wakiwa wanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya uanasheria Tanzania Tanzania (Law School of Tanzania -LST) watapaswa kurejesha mikopo hiyo kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Akizungumza wakati wakisaini mkataba wa makubaliano hayo leo Juni 21, 2022 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Bw.Abdul-Razaq Badru amesema kuwa Bodi hiyo imekuwa na uzoefu na utayari wa kutekeleza jukumu hilo na kuwakumbusha wanufaika hao kujitokeza na kurejesha.

"Tumejipanga kuanza kuwahudumia kuanzia Julai 1,2022 hivyo tunatoa wito kwa wateja wetu hawa kurejesha fedha hizi pamoja na zile walizokopeshwa wakiwa wanafunzi wa shahada za kwanza ili ziwanufaishe vijana wengine wa kitanzania wanaohitaji". Amesema Bw.Badru.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Jaji Dkt. Benhajj Masoud amesema wanasheria hao ni wale walionufaika na mikopo ya elimu wakiwa wanafunzi wa LST kati ya mwaka 2008 na 2015 wakisoma Stashahada ya Juu ya Uanasheria kwa Vitendo (Post Graduate Diploma in Legal Practice) wakati Sheria ya HESLB ilipokuwa hairuhusu wanafunzi wa LST kukopeshwa.

"Tunashukuru kuwa mikataba waliosaini walipokuwa wanafunzi -wanasheria ipo wazi kuwa LST inaweza kuipa kazi ya kukusanya madeni haya taasisi yoyote ya umma au binafsi na hivyo basi baada ya mazungumzo tangu 2019, leo tumefikia hatua hii". Amesema Jaji Dkt.Benhajj Masoud

Post a Comment

0 Comments