Ticker

6/recent/ticker-posts

JESCA SIMUCHILE ATOA ZAWADI MPYA KWA WAPENZI WA INJILI, “KAA NAMI BWANA” YATOKA



Msanii wa muziki wa Injili, Jesca Simuchile, ameendelea na safari yake ya kuhubiri kupitia muziki kwa kuachia rasmi wimbo wake mpya unaoitwa “Kaa Nami Bwana”, ikiwa ni kazi mpya inayokuja baada ya mfululizo wa nyimbo zake zilizogusa mioyo ya wapenzi wa muziki wa Injili.

Safari ya Jesca Simuchile katika kipindi hiki ilianza na wimbo “Tuimbe Tumepona” aliomshirikisha Ev. Daniel Safari, kazi iliyotolewa ikiwa na ujumbe wa matumaini, ushuhuda na kumshukuru Mungu kwa wema wake.

Baada ya hapo, Jesca aliendelea na kazi yake kupitia wimbo “Neema Ingalipo”, uliobeba ujumbe wa imani na matumaini, akisisitiza kuwa neema ya Mungu bado ipo kwa wanaomwamini na kumtumainia.

Agosti 2026, msanii huyo akaendelea na mfululizo huo kwa kuachia “Ndoa Iheshimiwe”, wimbo unaobeba mafundisho ya kibiblia kuhusu umuhimu wa kuheshimu, kulinda na kuthamini taasisi ya ndoa.

Sasa, Jesca Simuchile amerudi tena na “Kaa Nami Bwana”, wimbo mpya uliotolewa kwa mfumo wa Official Audio Music Lyrics, huku ukiwa na ujumbe wa kumwomba Mungu kukaa karibu na mwanadamu katika safari yake ya maisha.

Kupitia kazi hii mpya, Jesca anaendelea kuonyesha dhamira yake ya kutumia kipaji cha muziki kama chombo cha kufikisha ujumbe wa Injili, imani, matumaini na kumtegemea Mungu.

Kwa sasa, audio ya “Kaa Nami Bwana” tayari imeachiwa, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu video rasmi ya wimbo huo, ambayo inatarajiwa kuja baadaye.


SIKILIZA “KAA NAMI BWANA” HAPA:

Post a Comment

0 Comments