Ticker

6/recent/ticker-posts

MGAHAWA WA KFC WAZINDULIWA MAGOMENI DAR ES SALAAM

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule, Mkurugenzi Mtendaji wa Dough Works Limited, Vikram Desai na Viongozi wengine wakijata utepe kushiria uzinduzi wa Mgahawa wa KFC Magomeni jijini Dar es Salaam leo Februari 15, 2024.


MATOKEO mazuri ya sera, miundombinu, usimamizi ni chanzo cha kuvujitia wa wawekezaji hapa nchini.


Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule wakati wa Uzinduzi wa Mgahawa wa KFC katika Eneo la Magomeni Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Februari 15, 2024. Amesema kuwa Serikali ya wilaya ya Kinondoni itatoa ushirikiano mzuri katika ulinzi, Usalama na usafi ili waweze kutoa huduma bila kikwazo chochote.


Amesema kuwa vijana sio 40 wamepata ajira kufuatia kufunguliwa kwa mgahawa wa 10 hapa nchini hilo ni fahali kwa Tanzania kutokana na namna serikali ya Tanzania inavyofanya mazingira mazuri ya uwekezaji hapa nchini.


“Tunaona huduma zuri ya chakula inaenda kupatikana sasa Magomeni, watu wengi wanakuja kujifunza namna ya kutengeneza chipsi kutoka maeneo mbalimbali na kujifunza namna ya utoaji wa huduma inavyotolewa kwenye migahawa ya KFC hii ni fahari kwa watanzania kupata ujuzi mbalimbali.” Amesema


Dough Works Limited imetangaza ushirikiano wake na Kampuni ya Usambazaji wa Mafuta na Vilainishi ya vyombo vya moto ijulikanayo kama Total Energies wakati wa uzinduzi wa mgahawa wao wa 10 wa KFC uliofunguliwa katika Kituo cha Huduma ya Mafuta cha Total kilichopo Magomeni, Mapipa kwa lengo la kupanua wigo wa uwepo wa migahawa inayotoa huduma ya haraka ya Chakula nchini Tanzania.


Mkurugenzi Mtendaji wa Dough Works Limited, Vikram Desai amesema kuwa uzinduzi huo imekuwa ni miezi ya furaha na mafanikio kwa KFC na Dough Works kwa ujumla.


“Tukiwa tumeadhimisha Miaka 10 ya KFC nchini Tanzania na sasa kufungua KFC yetu ya 10 nchini kwa ushirikiano na Kampuni ya TotalEnergies ni hatua muhimu kwetu. KFC ni chapa ya kimataifa, na yenye maduka 23,000 katika zaidi ya nchi 140 duniani kote. Tunafurahi kuisambaza migahawa yetu ya KFC ulimwenguni kote na katika jamii zetu na kuendelea kutimiza ahadi yetu ya kutoa chakula chenye ubora na cha uhakika nchini Tanzania. Zaidi ya hayo, tunafurahi kuungana na mshirika mwingine ambaye atakuwa msaada mkubwa katika ukuaji wetu ambaye si mwingine bali ni TotalEnergies, na tunatarajia kufanya miradi mingine zaidi pamoja katika siku zijazo." Amesema


Kwa Upande wa Makamu wa Rais wa TotalEnergies kwa Afrika Mashariki na Kati, Olagoke Aluko, amesema kuwa Vituo vya TotalEnergies vitatambulika kwa kutoa huduma ya pamoja ambayo kwa sasa unaweza kushuhudia hilo katika kituo cha Magomeni ambapo mteja anaweza kupata huduma zote muhimu kutoka kwa huduma ya upatikanaji mafuta hadi huduma za gari, huduma za ATM na sasa huduma ya chakula cha haraka tena kile kinachopendwa na maarufu kwa sasa duniani kote na kufunguliwa kwa mgahawa huu ni ishara ya uwepo wa mgahawa wa KFC wa 10 nchini Tanzania.


“Ni jambo la kufurahisha na ukweli, nina shauku ya kuona huduma ya chakula kitamu na kizuri cha KFC cha kuku waliotongenezwa kwenye ubora wa hali ya juu ikianza kutolewa katika kituo hiki. Kama TotalEnergies, tunajivunia kuwa sehemu ya hatua hii na kutengeneza historia ya pamoja na mshirika wetu, Dough Works Limited. Kwa ofa nyingi ambazo KFC itatoa katika kituo hiki, ningependa kuwaalika kila mtu kutembelea KFC TotalEnergies Magomeni na kufurahia chakula cha kipekee na kinachovutia." Amesema


Amesema kuwa jumla ya migahawa 23 hutoa huduma kwa maelfu ya wateja kila siku kwa chakula cha mchana na jioni chenye ubora wa hali ya juu na chenye azma ya kukidhi mahitaji ya soko linalokua kila wakati, Dough Works imejitolea kuendelea kuongoza katika maendeleo ya ukuaji wa uwepo wa Migahawa yenye kutoa huduma ya chakula cha haraka na kinachopatikana kwa urahisi nchini Tanzania. Kwa sasa Dough Works Limited imeajiri zaidi ya wafanyakazi 700 na lengo ni kuendelea kufungua migahawa mingine zaidi ili kukuza fursa zaidi za ajira kwa Watanzania katika mikoa yote ya nchi. Mpango wa kuongeza migahawa mingine sasa unajumuisha miji ya Dodoma na Zanzibar.


Amesema kufunguliwa kwa KFC Total Magomeni, watumiaji sasa wanaweza kutembelea hapo na kupata huduma ya kupata chakula cha mchana na cha jioni cha kuku waliotengenezwa kwenye ubora mkubwa.

Dough Works Limited, ambao ni wa kwanza nchini Tanzania katika utoaji wa huduma ya chakula cha haraka na kufahamika kama wamiliki migahawa ya KFC na Pizza Hut nchini Tanzania pamoja na biashara yao nyingine inayokua haraka ya migahawa ijulikanayo kama BAO Café.

Post a Comment

0 Comments