Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Usimamizi Rasilimali Watu katika Taasisi za Umma-Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Hussein Kakurwa, akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Bodi ya Ushauri katika mafunzo elekezi ya Bodi ya OSHA yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha Mkoani Pwani.
****************
Na Mwandishi Wetu
Ofisi ya Msajili wa Hazina imesema Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ni miongoni mwa Taasisi muhimu kwa maendeleo ya Tanzania kutokana najukumu lake la msingi la kusimamia masuala ya usalama na afya katika maeneo ya kazinchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Usimamizi Rasilimali Watu katika Taasisi za Umma-Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Hussein Kakurwa, katika mafunzo elekezi kuhusu majukumu ya Bodi ya Ushauri ya OSHA yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha Mkoani Pwani.
“Kama tunavyojua suala la usalama na afya ni la msingi sana na ili Taifa lolote liweze kuendelea ni lazima lihakikishe watu wake wanafanya kazi katika mazingira salama na wanakuwa na afya njema. Kwahiyo jukumu ambalo OSHA wamepewa ni la msingi sanana Ofisi ya Msajili wa Hazina tunaichukulia OSHA kuwa miongoni mwa Taasisi nyeti naza kimkakati katika jukumu la serikali ya kusukuma maendeleo ya wananchi, ameeleza Kakurwa.
Aidha, amesema Ofisi ya Msajili wa Hazina inajukumu la kuendesha mafunzo kwa viongozi wa Taasisi za umma ili kuwafahamisha na kuwakumbusha kuhusu majukumu yao ya msingi kwa mujibu wa sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Mwenyekiti wa Bodi ya OSHA Bw. Makwaia Makani amewahakikishia wafanyakazi nchini kuwa Bodi yake itakuwa karibu na waajiri wote ili kuhakikisha kwamba wanaboresha mazingira ya kazi ili kulinda afya, usalama na ustawi wa wafanyakzi.
Ameongeza kuwa mafunzo elekezi waliyoyapata yamewapa fursa ya kuielewa kikamilifu Taasisi ya OSHA nahivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kusimamia na kufuatilia utendaji wa Taasisi hiyo.
Mjumbe wa Bodi hiyo, Bi. Rehema Ludanga, amesema baada ya mafunzo hayo niwajibu wao kama Bodi kutumia maarifa na uzoefu wao katika kumshauri Waziri na Menejimenti ya OSHA ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya msingi ya Taasisi.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa OSHA ambaye kwa mujibu wa muundo ndiye Katibu wa Bodi hiyo, amewashukuru viongozi wa juu kwa kuhakikisha Taasisi ya OSHA inapata Bodi mpya baada ya iliyokuwepo kuhitimisha kipindi chake.
“Tumekuwa na mafunzo mazuri sana ambapo wajumbe wamepitishwa katika sheria, mpango mkakati wa Taasisi na masuala mengine muhimu yanayohusu utendaji wa Taasisi yatu. Tunamshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri wetu, Mheshimiwa Deus Sangu kwa kuona umuhimu wa kuunda Bodi ili iweze kuishauri serikali kuhusiana na utendaji wa Taasisi hii,” amesema Mtendaji Mkuu na kuongeza:
“Na sisi tumeiahidi Bodi kwamba malengo yote tuliyoyaweka katika mpango mkakati wetu wa miaka mitano (2026-2031) ambayo yamezingatia vipaumbele vya Dira yaMaendeleo ya Taifa 2050 tutayatekeleza ipasavyo.”
Bodi ya Ushauri ya OSHA iliundwa hivi karibuni na kuzinduliwa rasmi Mei 25, 2026 JijiniDar es Salaam ambapo miongoni mwa majukumu ya msingi ya Bodi hiyo ni kumshauri Waziri mwenye Dhamana ya Masuala ya Kazi, Ajira na Mahusiano kuhusiana na utendaji wa Taasisi ya OSHA hususan katika kuandaa vipaumbele, mipango na bajeti pamoja na kufuatilia utekelezaji wa mipango hiyo ili kufikia malengo ya Taasisi.
Mwenyekiti wa Bodi ya OSHA Bw. Makwaia Makani, akifungua mafunzo elekezi ya Bodi ya Ushauri ya OSHA yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha Mkoani Pwani.
Mtendaji Mkuu wa OSHA, akiwasilisha salamu za OSHA katika ufunguzi wa mafunzo elekezi kuhusiana na majukumu ya Bodi ya Ushauri ya OSHA yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha Mkoani Pwani.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashariki, Dkt. Indiael Kaaya akiwasilisha mada kuhusu Mpango Mkakati wa OSHA wa miaka mitano (2026-2031)katika mafunzo elekezi ya Bodi ya Ushauri ya OSHA yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha Mkoani Pwani.
Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Usimamizi Rasilimali Watu katika Taasisi za Umma-Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Hussein Kakurwa (wakwanza kushoto), akijibu maswali na kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali katika mafunzo elekezi ya Bodi yaUshauri ya OSHA yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, KibahaMkoani Pwani.
Mwenyekiti wa Bodi ya OSHA Bw. Makwaia Makani, akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa Bodi hiyo, Bi. Rehema Ludanga, baada ya kuhitimisha mafunzo elekezi ya Bodi yaUshauri ya OSHA yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha Mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya OSHA Bw. Makwaia Makani, akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa Bodi hiyo, Bi. Lilian Dennis, baada ya kuhitimisha mafunzo elekezi yaBodi ya Ushauri ya OSHA yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha Mkoani Pwani.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya OSHA Bw. Makwaia Makani (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi hiyo. Wengine ni Bi. Rehema Ludanga (wakwanza kushoto), Bi. Khadija Mwenda (wapili kushoto), Bi. Lilian Dennis (wa kwanzakulia) na Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Usimamizi Rasilimali Watu katika Taasisiza Umma-Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Hussein Kakurwa mara baada ya kuhitimisha mafunzo elekezi ya Bodi ya Ushauri ya OSHA yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozicha Mwalimu Nyerere, Kibaha Mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya OSHA Bw. Makwaia Makani (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi hiyo na waratibu na wawezeshaji wa mafunzo elekezi ya Bodi ya Ushauri ya OSHA yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha Mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya OSHA Bw. Makwaia Makani (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi hiyo na baadhi ya Wawakilishi wa Menejimenti yaOSHA katika mafunzo elekezi ya Bodi ya Ushauri ya OSHA yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha Mkoani Pwani.










0 Comments